MICHEZO GENERAL

Amavubi Waichapa Stars 1 - 0

| Sunday, November 27, 2011
Waziri Mkuu Mizengo Pinda akiwapungia mikoni mashabiki
 kwenye uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam jioni hii,  Mara baada ya
kuzindua rasmi michuano ya TUSKER CECAFA CHALLENGE CUP 2011 ambapo leo
michuano hiyo imekutanisha timu za Tanzania Kilimanjaro Stars na Timu ya
 taifa ya Rwanda Amavubi,  mpira umekwisha na timu ya
Rwanda imeifunga Kilimanjaro Stars  goli 1-0 , katika picha kulia 
anayecheka ni Rais wa TFF na Shirikisho la Vyama vya michezo Afrika
Mashariki na kati CACAFA Leodger Tenga.
 Kikosi cha timu ya taifa ya Rwanda Amavubi kikiwa katika picha ya pamoja
Kikosi cha timu ya taifa yaTanzania Kilimanjaro Stars  kikiwa katika picha ya pamoja.
Mashabiki wa timu ya Kilimanjaro Stars wakiimba wimbo wa taifa kabla ya kuanza kwa mchezo huo kwenye uwanja wa Taifa.
Mshambuliaji wa timu ya Kilimanjaro Stars Mbwana Samatta  katikati akipiga mpira wa kichwa langoni mwa timu ya Amavubi huku mabeki wakijaribu kuzuia mpira huo usilete madhara golini mkwao.

Watanzania Wawili Kucheza Ligi Daraja La Pili Sweden

| Friday, November 25, 2011
Joseph Kaniki (Golota).
William John

Wachezaji wawili wa kitanzania, Joseph Kaniki (Golota) na William John wamefanikiwa kujiunga na timu ya ligi daraja la pili KonyaSpor (KIF) nchini Sweden, baada ya kufanikiwa kupita katika majaribio( Trials). Majaribio hayo yalijumuisha wachezaji zaidi ya thelathini ambapo wachezaji watano walichaguliwa kujiunga na klabu hiyo ya ligi daraja la pili KonyaSpor (KIF)Habari hii imeletwa kwenu na:http://www.africa4life.com/
Na Nancy Mtunga